Social Icons

Wednesday, August 10, 2016

LILIAN INTERNET KUSTAAFU UNENGUAJI ,BAADA YA KUTAMBA JUKWAANI KWA MIAKA 17

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Uongozi  wa  Kampuni  ya African  Stars Entertainment ( Aset), wanaomiliki bendi ya Twanga Pepeta wameandaa  usiku  maalum wa kumuaga  mnenguaji wake  mahiri LilianInternet katika onyesho lililopangwa kufanyika Agosti 27 mwaka huu .

Akizungumza na Blog hii leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji  pia  mmiliki wa beni hiyo Aset  Asha Baraka alisema kwamba tayari  wapenzi wa bendi hiyo  wameshapewa taarifa  za onyesho  hilo  hivyo  amewaomba wadau  mbalimbali  waweze kujitokeza siku hiyo kumuaga Internet.

"Internet ametumikia  jukwaani  kwa kunengua kwa miaka 17, hivyo  hivi sasa  umri umesogea  na yeye ni mama wa watoto wawili  ameamua kustaafu  ili aweze  kuitunza vyema familia yake   na maisha yake  atayaendeleza  kiujasiriamali"alisemaBaraka.

Itakumbukwa kwamba jina la Internet lilianza kusikika  akina anatumikia bendi ya Diamond Sound waliotamba na  miondoko ya Ikibinda Nkoi,baadaye alihamia Twanga Pepeta,baadaye Mashujaa ambako hakudumu akarudi tena  Twanga ambako  ndiyo anakomalizia safari yake ya unenguaji.
 Lilian akiwa jukwaani kwenye moja ya maonyesho ya bendi ya Twanga Pepeta

No comments:

 
 
Blogger Templates