Social Icons

Wednesday, August 31, 2016

DC NDEJEMBI AJIONEA KITUO CHA AFYA KILICHOJENGWA CHINI YA KIWANGO

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi waliofika kupatiwa huduma ya afya


Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deogratius Ndejembi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kituo cha afya Mlali


DcNdejembi alipotembelea wodi wa wagojwa
Dc Ndejembi akisisitiza jambo kabla ya kuondoka katika kituo cha afya Mlali

Na Mathias Canal, Singida

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deogratius Ndejembi amezuru katika kituo cha Afya cha Mlali kilichopo Katika Kata ya Mlali Wilayani humo kusikiliza kero wanazokumbana nazo wakati wanapofika hospitalini kupatiwa tiba.

Huu ni muendelezo wa ziara za kusikiliza kero za wananchi nakuzitatua kwa dhamira ya kupunguza na kuziondoa kabisa kero ndogo ndogo ambazo zimesababishwa na wananchi wenyewe ama watendaji wa serikali katika maeneo yote ya Wilaya hususani sekta ya Afya.

Mara baada ya kuwasili katika kituo hicho cha Afya alitembelea maeneo mbalimbali yakiwemo majengo mbalimbali, wodi, na Jengo la Upasuaji ambalo wameshindwa kulitumia kwa kutokana na kujengwa chini ya kiwango huku likiwa na eneo Dogo kiasi cha kupelekea kushindwa kuweka vitanda vya kutosha kwa ajili ya wagonjwa.

Licha ya jengo hilo kujengwa chini ya kiwango chini ya usimamizi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kabla ya Mkuu huyo wa Wilaya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kuhudumu katika Wilaya hiyo.

Hata hivyo kufuatia kadhia hiyo Mhe Ndejembi ameagiza Mkandarasi kutafutwa haraka iwezekanavyo ili aweze kuhakikisha jengo hilo linarekebiswa upwa kwa kutumia gharama zake mwenyewe.

Dc Ndejembi amemtaka mganga mkuu wa Kituo cha afya Mlali  kuhakikisha anasimamia vyema Mali na majengo ya umma ili kuendelea kutoa huduma nzuri na zenye ufanisi kwa kila Mtanzania anayefika katika Zahanati hiyo.

Kwa upande wa wananchi waliofika kupatiwa huduma kutoka katika Kijiji cha Mlale na maeneo Jirani wamesema kuwa huduma zinazotolewa katika Kituo hicho cha Afya zina ahueni kubwa huku changamoto kubwa ikiwa ni uduni katika huduma za chanjo kwa watoto kwani hawapati huduma hiyo kwa wakati.

Sambamba na hayo Dc Ndejembi ameagiza kusimamiwa haraka na kutatuliwa kwa kadhia hiyo ili wananchi wafurahie huduma bora zitolewazo katika vituo vya Afya sawia na kuimarisha Afya zao ili kufanya Kazi kwa salama na kuitikia dhana ya HapaKaziTu kwa vitendo.

No comments:

 
 
Blogger Templates