Social Icons

Wednesday, August 31, 2016

CHRISTIAN BELLA KUWASHA MOTO SHINDANO LA MISS KINONDONI 2016, KWENYE UKUMBI WA DENFRANCES

Washiriki wa shindano la  Lete Raha Miss Kinondoni 2016 wakishuka kwenye gari Dar es Salaam jana walipofanya ziara ya kutembelea Makao Makuu ya Mdhamini wao Kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd Mikocheni.
Wanyange hao 20 wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya 
gari la kampuni hiyo.
Meneja wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, Mr Rutha akizungumza na wanyange hao walipotembelea makao makuu ya Kampuni hiyo Mikochezni Dar es Salaam jana.
Warembo hao wakiwa mbele ya ghala zinamo hifadhiwa bia za Windhoek wakati wa ziara hiyo.
Warembo hao wakisubiri mkutano na wanahabari baada ya ziara hiyo.

Mshauri wa Miss Kinondoni, Boy George (katikati), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya shindano hilo. Kutoka kulia ni Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Mabibo,Constantine Mwafulilwa, Andrea Missana, Mratibu wa Shindani la Miss Kinondoni Rhamat George na Mwalimu wa warembo hao, Neema Chaky.
Maofisa wa Kampuni ya Mabibo wakiwa katika pozi. Kutoka kushoto ni, Mr Jerome, Ismail Mzava na Mr Rutha.
Mwalimu wa Wanyange hao, Neema Chaky (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Wanyange hao katika tabasamu.
Mratibu wa shindano hilo, Rhamat George (katikati), akizungumza katika mkutano huo.
Viongozim meza kuu na wanyange hao wakionesha bia ya windhoek.
Na Dotto Mwaibale
Mwanamuziki nguri wa muziki wa dansi hapa nchini Cristian Bella anatarajiwa kuwasha moto katika shindano la kumsaka Malkia wa Ulimbwende Kanda ya Kinondoni linatarajiwa kufanyika kesho kutwa Ijumaaya katika Ukumbi wa Denfrances Sinza jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kuwa kutanisha warembo hao  na wadhamini washindano hilo ambao ni Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd ambao ni wasambaji wa kinywaji cha Windhoek Dar es Salaam jana, Ofisa Mauzo wa kampuni hiyo, Andrea Misama alisema maandalizi ya shindano hilo yanaendalea vizuri ambapo aliwashukuru warembo wote waliojitokeza kwenye shindano hilo kwa mwaka huu na kuwa mwanamuziki huyo akishirikiana na kundi la sanaa la kampuni hiyo watapamba jukwaa kwa kutoa burudani la kukata na shoka.

"Mwaka huu washiriki waliojitokeza ni wengi ukulinganisha na mwaka jana, hivyo tunatoa pongezi kwa wazazi waliowaruhusu watoto wao kushiriki, malengo yetu ni kukuza vipaji na kutoa ajira kwa wasichana ili waweze kutimiza ndoto zao”,  alisema.

Kwa pande wao warembo watakaoshiriki shindano hilo wameahidi kuonyesha vipaji walivyonavyo na kuwaomba wadau na mashabiki waurembo kujitokeza kwa wingi siku ya shindano ili wawezekusapoti Miss Kinondoni.


Shindano hilo linashirikisha warembo 20 kutoka vitongoji mbalimbali vya Kanda ya Kinondoni ambapo kiingilio kitakuwa sh 10,000 na 20,000 kwa VIP huku shindano hilo likipambwa kwa burudani kutoka kwa mkali wa masauti Christian Bella.

No comments:

 
 
Blogger Templates