Social Icons

Sunday, July 10, 2016

TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBIMSIBA WA MWANDISHI WA HABARI ELIZABETH MAYEMBA


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Pinto kutokana na kifo cha Elizabeth Mayemba - Mwandishi wa Habari za Michezo wa Gazeti la Majira.

Rais Malinzi amesema, amepokea taarifa za kifo cha mwandishi huyo mwandamizi wa habari za michezo nchini kilichotokea Julai 09, 2016 na habari zake kuanza kusambaa majira ya jioni jana kabla ya kuthibitishwa na wanafamilia na uongozi wa TASWA kupitia njia mbalimbali za mawasiliano.

Marehemu alifariki dunia juzi  saa mbili usiku mwili wa marehemu utaagwa nyumbani kwake Tabata Kisukulu Jijini Dar es Salaam  leo na baadaye utasafirishwa kwenda kuzikwa katika makaburi ya Kola Mkoani Morogoro.

BWANA ALITOA  NA BWANA AMETWAA .

No comments:

 
 
Blogger Templates