Social Icons

Wednesday, July 27, 2016

TAMASHA KUBWA LA MUZIKI WA DANSI KUFANYIKA JUMAMOSI LEADERS CLUB

 Mkurugenzi wa Kampuni  ya  The African Stars Entertainment  AshaBaraka  akizungumza katika mkutano huo kuhusu tamasha hilo la kukata na shoka ambalo halijawahi  kufanyika hapa nchini.  Tamasha hilo limepangwa kufanyika Jumamosi Julai 30  2016 katika viwanja vya Leaders  Club, Jijini Dar es Salaam.
Picha Zote na Geofrey Adroph
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wanamuziki hao kuhusu tamasha hilo la muziki wa dansi nchini. Makonda amewapongeza walio buni wazo hilo huku akisema hata yeyeni mdau mkuu wa kuziki wa dansi huku akitoa ahadi ya kuwepo  siku ya onyesho hilo na kuahidi kutoa  zawadi ya Sh. Mil. 1 kwa bendi ambayo itakonga nyoyo za mashabiki watakao fika Leaders Jumamosi.

Mwanamuziki  Mkongwe wa muziki wa dansi, Ali Choki akiwaongoza wenzake kutoa burudani mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda walipofika ofisini kwake leo, kuzungumzia Tamasha la muziki huo litakalofanyika Jumamosi  Viwanja vya Leaders ambalo litashirikisha bendi 10 maarufu za hapa nchini.

Baadhi ya waandishi wakiwa kazini
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wanamuziki wa dansi baada ya kuzungumza nao ofisi kwake.

No comments:

 
 
Blogger Templates