Social Icons

Sunday, October 4, 2015

WATANZANIA WAASWA KUWAPELEKA WATOTO WAO KATIKA SHULE YA SEKONDARI IMPERIAL ILIYOPO CHALINZE MSOLWA, MKOANI PWANI



Wanafunzi wa kidato cha kwanza wa Shule ya Sekondari ya Imperial wakielekea kupandisha bendera ya Taifa wakati wakisherekea mwaka mmoja wa shule hiyo iliyopo Chalinze Msolwa mkoani Pwani.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Imperial wakiwa  ndani ya darasa la Komputa

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Imperial wakijibu maswali ya kuhusiana na komputa katika darasa hilo.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Imperial, Ivonne Mnyitafu akitoa ufafanuzi kwa wazazi pamoja na walimu wa shule hiyo.
Mwalimu wa Taluma  wa Shule ya Sekondari ya Imperial, Peter Mwanda akizungumza katika siku ya Imperial iliyofanyika leo katika shule hiyo iliyopo Chalinze Msolwa mkoani Pwani.

Wazazi wakiwasikiliza wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Imperial wakati wa kusherekea siku ya Impirial iliyofanyika Shuleni hapo leo.
Wazazi waliowatembelea wanafunzai wa shule ya Sekondari Imperial wakielekea katika chumba cha masomo ya Sayansi (Laboratory) wakati waliposherekea siku ya Imperial iliyofanyika leo katika shule hiyo iliyopo Chalinze-Msolwa mkoani Pwani.
wanafunzai wa shule ya Sekondari Imperial wakifanya majaribio ya masomo ya Sayansi ambayo ni Fizikia pamoja na Kemia katika chumba hicho cha majaribio ya masomo hayo shuleni hapo leo.
Mkuu wa Shule na Mkurugenzi Mtendaji wa shule ya Sekondari Imperial, Arup Mukhopadhyay akitolea ufafanuzi moja ya kifaa kinachotumika kuchuja maji ambayo yamechanganywa na mchanga mbele ya wazazi na walezi waliofika shuleni hapo kwaajili  ya siku ya Imperial iliyofanyika leo shuleni hapo.
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Sekondari Imperial,Buhela Lunogelo akiwapongeza kuwapongeza wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya kufanya majaribio ya masomo ya Kemia na Fizikia shuleni hapo leo.Kulia ni Mkuu wa Shule na Mkurugenzi Mtendaji wa shule ya Sekondari Imperial, Arup Mukhopadhyay.
Baadhi ya wazazi wakichukua kumbukumbu zao (Taswira mbalimbali) wakati wanafunzi wa shule hiyo wakifanya majaribio ya masomo ya Fizikia na Kemia katika chumba hicho katika shule ya Sekondari Imperial leo.
Baadhi ya wanafunzi  shule ya Sekondari Imperial wakifafanua somo la hesabu la pembe zinazoundwa na pembe tatu mbele ya wageni waalikwa na wazazi au walezi wao (hawapo pichani) waliohudhulia katika siku ya Imperial iliyofanyika Chalinze Msolwa mkoani Pwani leo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Imperial wakifanya mdahalo katika siku  Imperial iliyofanyika leo katika shule hiyo.
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Sekondari Imperial, Buhela Lunogelo akizungumza na waandishi wa habari leo katika shule hiyo kuhusiana na maendeleo pamoja na uzuri wa taaluma inayotolewa katika shule hiyo kuwa ni ya kimataifa, aidha amewaomba wazazi wenye watoto wanataka kusoma kidato cha kwanza mpaka cha nne wawapeleke watoto wao katika shule hiyo iliyonzishwa Machi 3 Mwaka huu.
 Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Sekondari Imperial, Buhela Lunogelo akiwapa zawadi wanafunzi wa shule hiyo leo Chalize Msolwa Mkoani Pwani, kushoto ni Mkuu wa Shule na Mkurugenzi Mtendaji wa shule ya Sekondari Imperial, Arup Mukhopadhyay.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Imperial wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa na vikombe na vyeti vyao walivyozawadiwa leo
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Imperialwakitoa burudani katika siku ya Imperial iliyofanyika leo mkoani Pwani.

No comments:

 
 
Blogger Templates