Social Icons

Tuesday, September 1, 2015

DC .PAUL MAKONDA KATIKA UZINDUZI WA VITABU VYA MWL. LILIAN NDEGI

Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mh.Paul Makonda siku ya jana katika kanisa la Living Water Center chini ya mtumishi wa Mungu Apostle Onesmo Ndegi alikuwa mgeni wa heshima katika uzinduzi wa vitabu vitatu  "MJUE MWANAMKE,USIIPE HOFU NAFASI na RAFIKI ANAYEKUFAA vilivyoandikwa na Mwl Lilian Ndegi wa Kanisa la Living Water Center Kawe.

Ibada hiyo ya uzinduzi wa vitabu ilipambwa na vikundi vya uimbaji sifa kama Living Waters wenyeji Upendo Nkone,GUG Dancers na More Than Enough Band.


Mkuu huyo wa wilaya ndiye aliyezindua vitabu hivyo na kuendesha zoezi zima la uuzaji wa vitabu hvyo,kwa kuanza alinunua vitabu hivyo vitatu kwa shiling Milioni 5 ikiwa ni kuchangia na kusapoti huduma hiyo ya uandishi wa vitabu vya Mwl Lilian Ndegi ambaye ni Mama yake kwa malezi ya kiroho kanisani hapo Living Water Center Kawe.


Katika uzinduzi huo uliambatana na kukata keki ikiwa ni ishara ya kufurahia mafanikio ya kazi ya uandishi wa Mwl Lilian Ndegi na ugawaji wa zawadi katika tukio hilo ulifanyika kwa watu ambao wamekuwa wakihusika katika ufanikishaji kwa namna moja au nyingine au kumuwezesha Mwl Lilian kufanikisha uandishi wake wa vitabu.


Mh Paul Makonda aliwasihi washirika wa Kanisa la Living Water Center Kawe kusapoti kazi ya Mwl Lilian ikiwa ni kwa kununua na kuvisambaza vitabu vyake ili viwafikie wasomaji wengi ikiwa vitaleta matokeo mazuri katika maisha yao kutokana na ujumbe ulio ndani ya vitabu hivyo.


Apostle Onesmo Ndegi kiongozi wa Kanisa la Living Water Center na mme wa mwandishi wa vitabu Mwl Lilian Ndegi katika kuzungumza kwake alikuwa akijivunia Mkuu huyo wa Wilaya na kusema ni kijana wake anamfahamu vizuri siku nyingi tangu bado anasoma na kusema amelelewa hapo na kusema kuwa alikuwa msikivu,na mpaka Mh Rais kumteua kwa nafasi hiyo ya kuwa Kiongozi wa Wilaya hakukosea.


Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mh.Paul Makonda alipokuwa akizungumza baada ya kuzindua vitabu 
Mh.Paul Makonda akizindua vitabu 
 Mh.Paul Makonda alipokuwa akionesha vitabu baada ya kuzindua
Apostle Ndegi akimlisha keki Mwl Lilian Ndegi ambaye ni mke wake ikiwa ni ishara ya kupongezana
Mh.Paul Makonda akilishwa keki Mwl Lilian Ndegi mwandishi wa vitabu vilivyozinduliwa
Baadhi ya wageni waliokuwa wamealikwa katika uzinduzi huo wa vitabu wa kwanza kush Mchungaji Deborah Ntepa,Mama Mchungaji Tumwidike koka Mbeya na Mwl. Lilian ndegi mwenyeji
Mh.Paul Makonda alipokuwa akiwakabidhi vitabu baadhi ya watu walionunua baada ya kuvizindua
Mh.Paul Makonda alipokuwa akiwakabidhi Mzee wa Kanisa vitabu baadhi ya watu walionunua baada ya kuvizindua
Mh.Paul Makonda alipokuwa akiwakabidhi Kiongozi wa mabinti Kanisani hapo Magreth vitabu baada ya kuvizindua

Mama Mchungaji Tumwidike kutoka mbeya alikuwepo katika uzinduzi huo
Mchungaji Deborah Ntepa kutoka Oasis Healing Ministry alikuwepo katika uzinduzi huo
Upendo Nkone alipokuwa akihudumu katika ibada ya uzinduzi wa vitabu iliyoongozwa na Mh. Makonda

Mwl Lilian Ndegi na Upendo Nkone wakicheza mbele za Bwana ilikuwa full shangwe
Mh.Paul Makonda wa kwanza kushoto,katikati ni Apostle Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center na wa mwisho ni Mwandishi wa vitabu Mwl. Lilian Ndegi 
Mh.Paul Makonda na Mwandishi wa vitabu Mwl. Lilian Ndegi katika picha ya pamoja baadhi ya mabinti  wa kanisani hapo.
Mwandishi wa vitabu Mwl. Lilian Ndegi katika picha ya pamoja baadhi ya wakina mama wa  kanisani hapo.

No comments:

 
 
Blogger Templates