Social Icons

Monday, March 2, 2015

MAMIA WATOA HESHIMA YA MWISHO KWA KEPTENI JOHN DAMIANO KOMBA

Wasanii wakongwe wakiimba wimbo ambao awali uliimbwa na marehemu alioutunga kwa akiji ya kifo cha Hayti baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere lakini wao wakaubadilisha maneno na badala ya Nyerere waliimba Komba (Picha Zote na Francis Dande)
Wanamuziki wa kizazai kipya nao hawakubaki nyuma waliimba kama ishara ya heshima kwa Komba
 Rais wa Awamu ya pili , Alli Hassan Mwinyi akitoa heshima ya mwisho.
 Rais Jakaya Kikwete akipia  kwenye jeneza la mwili wa marehemu  Kepteni Komba.
 Famila ya marehemu Komba wakiwa wameketi  nyuma ya jeneza.
 Hapa wakiweka mambo sawa kwa ajili ya  kutoa heshima za mwisho.
 Baadhi ya wasanii waBongomovie ambao walijitokeza  na kuimba wimbo wa kumuaga Komba.
 Mbunge wa Kinondoni Mh. Idd Azzan wakwanza kulia akiwa  katika viwanja vya Karimjee.
 Wasanii wakongwe wakiongozwa na King Kiki , , Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,Luizer Mbutu, Kalala Junior na Jose Mara wakiimba kwa uchungu wimbo ambao uliwaliza wengi waliohudhuria kwenye  hafla hiyo.
 Rais Jakaya Kikwete akifuta  chozi kutokana na mashairi ya wimbo huo ambao awali uliimbw ana marehemu komba ukiwa kati ya nyimbo zake alizotunga wakati wa msiba wa Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere.
 Familia ya Komba wakilia kwa uchungu leo.
 Mbunge wa Viti Maalum CCM ,Matha Mlata wakwanza kushoto  akiwa na baadhi ya viongozi .
 Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete akitoa heshima zake za mwisho kwenye jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu Kepteni Komba.
 Rais wa Awamu ya tatu Benjamin Mkapa akitoa heshima za mwisho katika mwili wa marehemu
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Anne Samamba Makinda akitoa heshima za mwisho
 Katibu Mkuu wa Chama tawala Chama Cha Mapinduzi ,Abdulrahman Kinana akitoa heshima za mwisho kwa  mwili wa marehemi Komba.
 Aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Ngoyayi Lowassa akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Komba.
 Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Yusuph Makamba akipangusa machozi.
 Makamu wa Rais Dkt.Gharib Bilal akitoa heshima zake za mwisho
 Mama Anna Mkapa naye alikuwepo.



 Aunt Caroline Sanga wa kwanza kushoto mwenye nyeusi, Mke wa marehemu mama Salome Komba anayefuata wakiwa katika viwanja vya Karimjee, Jijini Dar es Salaam.
 Khadija Kopa wapili kushoto  akiwa msibani
 Baadhi ya watu wakiwa katika viwanja vya Karimjee ambako walihudhuria  hafla hiyo
Mjane wa marehemu akibusu mwili wa mume wake marehemu Kepteni John Komba.Marehemu Komba atazikwa kijijini kwao kesho Lituhi mkoani Ruvuma.
 
NA KHADIJA KALILI
“NDUGU  Wanzania, leo yametimia yaleyaliyoandikwa na mwenyeezi Mungu, Kiumbe mwadilifu na kipenzi cha watu, Kepteni Komba leo ametuacha ooh kepteni Komba ooh kwaheri baba, ooh Kepteni Komba kwaheri baba.”

Hii ni sehemu ya shairi lililoimbwa jana na wasanii wa muziki wa dansi wakiongozwa na King Kiki akiwemo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, wakati wa kuaga mwili wa Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba katika Ukumbi wa Kareemjee, jijini Dar es Salaam.
Kapteni Komba aliyefariki dunia jioni ya Februari 28, mwaka huu, mbali ya kuwa mwanasiasa, ni ni mwalimu kitaaluma na msanii mahiri mwenye kipaji cha aina yake katika uimbaji ikiwemo uwezo wa kutunga nyimbo mbalimbali za kisiasa na kiharakati kwa kipindi cha uhai wake.
Hata kibao hicho kilichoimbwa jana na mzee King Kiki na wasanii wengine wakati wa kuagwa kwa mwili wa Komba na kuwaliza wengi akiwemo Rais Jakaya Kikwete, kilitungwa naye kuomboleza msiba wa Baba wa Taifa, Mwl. Julius K. Nyerere aliyefariki Oktoba 14 , 1999.
Alichofanya King Kiki na nguli wenzake akiwemo Jose Mara, Luizer Mbutu,  Kalala Junior, Abdul Salvador ‘Father Kidevu,’ Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Matha Mlata na Nape, ni kutumbukiza jina la marehemu (Komba) badala ya Nyerere.
Kwa mguso wa kibao hicho ambacho kiliwahi kuwaliza wengi na kutikisa vilivyo wakati wa msiba wa Baba wa Taifa, aina ya maneno yaliyomo ndani yake na ujumbe ulioendana na mazingira ya msiba huo, jana vilitosha kuwaliza tena wengi akiwemo Rais Kikwete kwa kushindwa kuvumilia.
Maneno yaliyotamkwa na Nape kwa staili ya kughani yasemayo ‘nenda Komba kamsalimie baba wa Taifa, Simba wa Vita (Rashid Kawawa) waambie  wameacha  historia ya kutukuka, waliombee taifa letu kwa kipindi hiki, ni maneno yaliyoibua hisia na simanzi kali kwa umati uliojitokeza. 
Wakati taratibu za kuaga mwili, baadhi ya watu mbalimbali wakiwemo wasanii, walielezea kuguswa na msiba huo kubwa zaidi ni pigo kubwa kwa tasnia ya muziki na sanaa kwa ujumla kutokana na mchango wa Komba wakati wa uhai wake.  
Kwa upande wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata)   Godfrey  Mngereza, alisema Komba alikuwa ni sawa na mwalimu wa sanaa na kioo cha wasanii wengi nchini ikiwemo  Chuo Cha Sanaa Cha Bagamoyo.
“Tanzania One Theatre (TOT), walikuwa wakija kupiga kambi Bagamoyo, hivyo aliweza kuchukua wasanii wengi wasomi wa Bagamoyo na kuviendeleza vipaji vyao,” alisema Mngereza na kuongeza kuwa, ni kifo kilichoacha pengo kubwa kwa taifa.
Naye Matha Mlata, amesema ni kifo kilichowagusa wengi na kuwasihi wasanii wamuunge mkono Mkurugezni atakayeteuliwa kukiongoza kikundi cha  Tanzania One Theatre (TOT), kwa kumpatia ushirikiano katika kuenzi mchango wa marehemu Komba.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wasanii Tanzania (SHIWATA), Tallib Cassim alisema wamepoteza kiongozi na mhimili wa shirikisho kwa sababu alikuwa ni Makamu Mwenyekiti wa Shiwata, hivyo anafahamu mchango wake wa ndani na nje ya shirikisho hilo.
Talib alisema, Komba alikuwa mtetezi wa Shiwata hata alipokuwa Bungeni akielezea malengo ya uwepo nwa chombo hicho kwa wabunge wengi hadi wakaelewa, hivyo kuwa mwanzo wa kupata baraka zote.

Amewasihi wasanii kuungana wakiwa na chombo kimoja kitakachowasemea na kupigania maslahi yao akisema kwa kukosa umoja thabiti, jana walikosa msemaji rasmi wa wasanii katika msiba huo.
Naye Sylvester Mujuni ‘Mpoki’ msanii wa vichekesho naye amemlilia  Komba kwa kusema msiba ni jambo lenye simanzi siku zote, hivyo yeye kama msanii ameumia huku akisema kuna wakati alikwaruzana na Komba kutokana na jinsi alivyokua akimuigiza katika vichekesho vyao vya Komedi.
Mpoki alisema, hata yeye alipokuwa akimuigiza, hakua akifanya kwa nia mbaya ni suala la sanaa jampo ambalo kuna wakati Komba alikua anakasirika, lakini baadaye akakubaliana na hali halisi.

“Lakini, mwisho wa siku Komba alikuwa akinielekeza kuwa nisimuigize nikiwa mchafu si unajua sisi wasanii wakati mwingine tunaigiza huku tukiwa hatujapiga nguo pasi, akanitaka niweke ndevu, kitambi na nivae ‘smart’ na mimi nilifanya hivyo,” alisema Mpoki.
Naye Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana alimwagia sifa kemkem Komba kwa kusema , nyimbo zake zilikuza uzalendo  katika nchi hii. “Nyimbo za Komba zilileta changamoto kubwa kila ziliposikika  kifo chake ni pigo kubwa kwa wasanii,” alisema kwa simanzi kubwa.
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama aliyechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa muziki wa injili kupitia uratibu wa matamasha ya Pasaka na Krismasi, alisema kifo hicho ni pigo na pengo kubwa kwa taifa ambalo ni gumu kuzibika. 

Alisema nje ya sanaa, Komba ni mtu ambaye hakuwa na uroho wa madaraka kwani pamoja na kupata umaarufu mapema wakati wa Serikali ya Awamu ya Kwanza, alisubiri hadi mwaka 2005 alipogombea Ubunge.
Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan alisema kifo cha Komba ni pigo kwa tasnia nzima ya muziki wa dansi akisema anamkumbuka sana kwani wakati anaanzisha bendi yake ya Pamo Sound, ndiye alikua mshauri wake.
“Kubwa zaidi ninalomkumbuka Komba ni jinsi alivyouinua muziki wa taarab ambapo kama watu watakumbuka, ulikuwepo ushindano mkubwa kati ya TOT Taarab na Muungano ambapo wasanii wa kike Khadija Kopa na Nasma Kidogo  (marehemu), walikuwa ni mahasimu wa jukwaani,” alisema.                                                              



No comments:

 
 
Blogger Templates