Social Icons

Friday, March 6, 2015

KOMBA AMWACHIA ASHA BARAKA SIRI NZITO,ALIWAAGA MISAMBANO NA THABIT ABDUL

 SIKU  chache za uhai wake aliyekuwa Mkurugenzi wa Tanzania One Theatre (TOT), marehemu Kapteni John Damino Komba aliweza kuuwaaga baadhi ya wasanii wa TOT kwa kuwasisitiza wafanye mazoezi ya nyimbo zake mpya.

Marehemu Komba aalimpigia simu Abdul Misambano mwimbaji wa taarabu ambaye aliweza kufahamika kwa jina la ‘Asu’ kutokana na kibao chake amvcho hata kikipigwa leo bado kitaamsha hisia za msikilizaji.

Komba alimpigia simu Misambano na kumsisitiza aende mazoezini kadhalika alifanya hivyohivyo kwa Thabit Abdul ambaye ni kati ya wapiga kinanda mashuhuri nchini wote kila  kila mmoja alimtumia fedha kwa njia ya Tigo Pesakiasi cha sh. 100,000 ambazo marehemu alisema watumie kama nauli zao wanapokwenda mazoezini.

Lakini kabba wasanii hao hawajazitoa wala kuzitumia ndipo ghafla wakapata taarifa kuwa Mkurugenzi  Komba wao amefariki dunia  na mazoezi hayakufanyika tena. 

Aidha hakuna mtu aliyetarajia kama Mkurugenzi wa Kampuni ya The African Stars  Twanga Pepeta (ASET),  Asha Baraka ndiye aliyeandika mashairi ya wimbo ule ambao uliimbwa kwenye hafla ya kumuaga aliyekuwa Komba.
“Mimi nilikua katika Kamati ya burudani ambayo ilikuwa ikisimamiwa na Mmoja wa Wakurugenzi wa Clouds Media Ruge Mutahabapia hivyo nikapewa jukumu la kuwakusanya wasanii ili waweze kutunga wimbo wa kuimba siku ya kuuga mwili wa marehemu komba” anasema Asha.
Anaendelea kwa kusema kuwa lakini mara baada ya kuona wasanii wanasumbua akaamua kuutumia wimbo wa marehemu Komba aliouimba katika msiba wa  Hayati baba wa Taifa Julius Nyerere  kwa kutoa sifa zilizokuwa zikimuhusu Nyerere na kumtaja Komba.
Hivyo nikawambia wasanii wakiongozwa King Kiki ‘Wazee Sugu’ wasiumize sana vichwa vyao kwa sababau wanaweza kukopi nyimbo za Komba kwa ni nyingi.
Hivyo baada ya yeye  kuandika mashairi hayo na kumwonyesha Ruge  akayakubali wasanii wakafanyia mazoezi na kuingia studio, ambapo gitaa la rhythm na solo lilipigwa na Miraji Shakashia wa Twanga Pepeta huku sauti ya kinanda ikiingizwa na Abdul Salvador  (Father Kidevu)pamoja na Nape Nnauye (CCM).
“Hilo lilikwa ni wazo langu hivyo ndiyo sababu kubwa iliyopelekea wasanii kutotunga wimbo mpya wa kumuenzi Komba hivyo wakaamua kuupa jina la ‘Nani Huyo’ ”anasema Asha.

Asha  amefunguka zaidi  namna walivyofahamiana na Komba katika  enzi za uhai wake.
Asha anaaza kwa kusema “mimi nilifahamiana na Komba mwaka 2000 ambapo Komba aliniandikia barua  ya kumuomba aliyekuwa mwanamuziki wa Twanga Pepeta kwa wakati huo Ramadhani Masanja  (Banzastone).

“Nakumbuka wakati huo nchi ilikuwa katika kuelekea kipindi cha uchaguzi mkuu hivyo nilienda ofisini kwake TOT CCM Mwinjuma Mwananyamala, Jijini Dar es Salaam tukakubaliana  amchukue Banzastone na mara baada ya kampeni atamrudisha  twanga lakini hakurudi”.
Anaongeza kwa kusema kuwa Banza akachukuliwa kwa dau nono  na  kutokana na kukaidi kwake kumrudisha tukaingia kwenye mgogoro lakini baadaye tukaja kuzunguma yale ya kaisha na kazi zikaendelea kama kawaida.
Asha anaendelea kwa kusema kwamba nakumbuka Komba ndiye aliyechangia kuupandisha muziki wa dansi nchini ambapo walikuwa wakifanya kazi kwa ushindani  katika muziki, huku wote wakiwa kitu kimoja katika kufanya kazi ambapo kwa mara ya kwanza wote kwa pamoja wakakubaliana kuandaa mpambano wa nani zaidi kati ya TOT na Twanga huku mpambano huo ukiwa wenye kuvuta hisia za mashabiki wa wadau mbalimbali wa muziki wa dansi  na wa bendi hizo mbili.

Asha anasimulia kwamba onyesho hilo kubwa lilifanyika kwenye ukumbi wa Vijana Hostel Kinondoni.
Asha anasema uhusiano wao mzuri ulidumu hata baaada ya kuingia kwenye ulingo wa siasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo walikuwa wakikutana katika chaguzi mbalimbali za kisiasa.
Asha anaongeza kwa kumwelezea Komba kwa kusema kwamba  hawakuishia hapo tu bali wao Twanga wakawa wanapata nafasi ya kuomba jukwaa na hata vyombo vya TOT  pale walipoomba kutumia huku marehemu akimwambia asha atafute usafiri wa kubebea vifaa  hivyo.
Kama hiyo haitoshi Asha anasema kwamba ana siri nzito aliyoachiwa siku chache kabla ya kifo cha Komba .
“Siku chache kabla hajafariki marehemu Komba tulikutana soko la TX Kinondoni hivyo alifurahi kuniona pale na kuingia katika gari langu hapo ndipo tulipozungumza mambo mengi saana huku yeye akiwa ni mzungumzaji zaidi ambapo  alianieleza matatizo yake na changamoto nyingi anazokutana nazo na jinsi anavyokabiliana nazo, tulikaa kwenye gari yangu tukazungumza  ila kilichotukatisha ni kukatika kwa mafuta  ya gari hivyo AC ikakata akanipa sh. 20,000 ili nimtume kijana na kidumu akaninunulie  mafuta tukaachana hapo baada ya siku chache kupita Jumamosi Februari 28 alasiri ndipo nikapigiwa simu kafariki dunia nimeumia sana” anasema Asha.

Mbali ya kuzungumza na marehemu siku chache  na za mwisho za uhai wake Asha anasema kwamba atapata taabu kwa mazoea aliyokuwa nayo walipokuwa  kwenye vikao vyao vya Kamati Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi NEC (CCM),Dodoma ambapo wajumbe wa mikoa ya Ruvuma na Kigoma hukaa karibu hivyo atakapokiona kiti cha marehemu Komba kitambumbusha namna alivyokuwa mcheshi wakati wa kikao kikiendelea na walivyokuwa wakitaniana.

“Nakumbuka mara ya mwisho katika kikao cha NEC ,Dodoma aliniita akanieleza  matatizo yake lakini hayo ni siri yangu mimi” anasema Asha. 

Nitakapoingia katika ukumbi nitakiona kiti chake  roho itaniuma sana  sababu tulikua tunakaa karibu hivyo nafasi yake nitaiona imepwaya ndani ya ukumbi.

Akimzungumza kwa upande wa burudani anasema marehemu Kapteni Komba TOT ameandika historia ya bendi hiyo kwa kuiendesha kwa umakini wa hali ya juu .

Hilo lilijidhihirisha kwa jinsi alivyofanikiwa kuendeleza muziki wa taarab, kwaya na muziki wa dansi.

“Pia Komba alikuwa na vikundi vingi vidogovidogo ambapo vijana walikuwa wakikusanyika na kuonyesha vipaji vyao ambavyo baadaye viliendelezwa” anasema Asha.

Anaongeza kwa kusema kuwa katika kuonesha kwamba yeye hana ubaguzi aliweza kuwaajiri wacheza shoo wenye ulemavu wa miguu ambao nao hawakufanya ajizi pale walipopewa nafasi walicheza vizuri mtindo wa ‘Achimenegule’.

Asha anatoa angalizo kwa uongozi wa CCM ambao ndiyo wanamiliki kundi la TOT, kwa kusema kwamba anawaomba wafanye uteuzi kwa mtu mwenye  moyo ili aweze kuendeleza mema yote yaliyoanzishwa  na Marehemu komba.

“Komba alikuwa jabali nani asiyemtambua  kwani hata watoto wadogo walifanikiwa kuziimba nyimbo za TOT kwenye michezo yao kama vile achimenengule”anasema Asha.

Naye mwanamuziki Kalala Junior anavyo mlilia Kapteni Komba  ambaye kwa sasasa ni mwanamuziki wa bendi ya Twanga Pepeta anasema kuwa Kapteni Komba alikuwa ni kama baba yake kwa sababu hata wakati akiitumikia bendi ya TOT alimchukulia kama mtoto wake  na yeye akijiona kana kwamba yuko kwa babake mzazi.

“TOT ilikuwa bendi yangu ya pili hivyo sikuona taabu yeyote kuwa katika bendi ile kwani nilikuwa bado kijana mdogo (20) kwa wakati huo” anasema Kalala.

Kalala aliongeza kwa kusema kuwa amepata pigo kubwa sana lakini hakuna njia ila kumshukuru mungu kwa kila jambo.

“Kapteni Komba alikuwa ni mshauri wangu mkuu katika maisha yangu na kila wakati nilikuwa napita TOT kumsalimia na kuchukua busara zake”anasema Kalala.

Anaongeza kwa kusema kuwa hata alipokuwa akihama hama bendi alimsema hivyo aliposikia amerudisha mizigo yake katika bendi ya Twanga Pepeta akamwambia nilijua huko kote ulikuwa ukihangaika tu sasa hapo utulie.

Naye Mchumi wa Wachumi wa Wilaya ya Kinondoni Yusuphred Mhandeni  ambaye pia ni mdau mkubwa wa bendi za muziki wa dansi hapa nchini aliongezea kwa kusema kuwa msiba wa Komba ni pigo kwa taifa kwani Komba amechangia katika kukuza muziki wa dansi nchini na kuufikisha hapa ulipo sasa.

Kama itakumbukwa Komba ndiye aliyeanzisha mtindo wa kununua wanamuziki kwa bei ya juu hivyo hadi hapo utaona aliupa hadhi muziki nz wanamuziki pia .

“Aliweza kuwaajiri TOT  kwa nyakati tofauti wanamuziki wakubwa watatu ambao ni mafahari watatu  kama Banzastone, Ally Choki na Muumini Mwinjuma” anasema Mhandeni

Muziki wa dansi una vipaji vitatu ambavyo ni Muumini, Choki na Banzastone wote hawa Komba aliweza kuwamiliki .

Mhandeni anamalizia kwa kusema kuwa siyo siri kwa upande wa siasa CCM wamepata pigo kwani Komba alikuwa na kipaji cha kuhamasisha katika kampeni.

Tumepoteza kipaji ambacho kukipata itakuwa kazi na labda mtithi wake atazaliwa na vizazi vijavyo siyo sasa.

Mwisho.
Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa Email :lindashebby@gmail.com 0755707046

No comments:

 
 
Blogger Templates