Social Icons

Tuesday, September 23, 2014

MKOLANI FC WAIBUKA KIDEDEA PEPSI MEYAS CUP 2014 MWANZA

 Mabingwa kabla ya mechi wakiwa katika picha ya pamoja.
 
 
 
 
 
 Mashabiki waliojitokeza licha ya kupata burudani ya kandanda pia walipata  ngoma ya asili.
 Meza kuu.
 Mahsbiki wakipagawa na mechi.
 Hii ndiyo Bajaj iliyotolewa  na Kampuni ya vinywaji baridi ya Pepsi kama zawadi kubwa kwenye michuano hiyo.
 Mashabiki wakiwa wamejaa kwenye uwanja wakishuhudia mpambano huo.
 
  David Albert kutoka Kituo cha Alliance na kupata sh . 200,000  huku timu ya Kata ya Mahina FC ikipata ikiibuka kuwa timu bora na yenye nidhamu na kuondoka na zawadi y ash. 200,000.
  Paulo Godfrey akiwa na bao nane alijinyakulia kiatu cha dhahabu na  fedha kiasi cha sh.200,000.
 Washindi wa Pili wakipokea zawadi yao ya Kombe na fedha.
 Hapa ikining'inizwa funguo ya Bajaj ambayo imekwenda kwa washindi wa michuano hiyo.
 Bingwa Mkolani FC akipokea Kombe la ushindi wa michuano hiyo ya Pepsi Meyas Cup Mwanza.
 Wachezaji wa Mkolani FC wakishangilia ubingwa huku wakinyanyua Kombe la ushindi.
TIMU ya Kata ya Mkolani FC imeibuka Mabingwa wapya wa Kombe la Meya 2014 baada ya kuichapa timu ya Kata ya Mirongo bao 2-1 jumamosi iliyopita katika mchezo wa fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Awali katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu ulioanza mapema saa 8:00 mchana kwa timu ya Sokoni FC kuichapa Mnadani FC bao 3-0 na kuibuka mshindi wa tatu wa michuano hiyo huku magoli ya Sokoni yakifungwa na Joseph Mwajalila dakika 33 kwa penati na Salimu Hamis dakika 39, 51na kuwapa tiketi ya ushindi wa tatu.
Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu Mratibu wa michuano hiyo Paul Mganga alisema fainali hiyo iliyoshuhudiwa na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo aliyeambatana na Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa, muasisi wa mashindano hayo Mstahiki meya wa Jiji la Mwanza, Stanclaus Mabula, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halifa Hida, Mwenyekiti wa Chama cha soka Mkoa wa Mwanza (MZDFA), Jackson Songola na Katibu wa MZDFA, Nasibu Mabrouk.
Ndikilo alisema mashindano hayo yamewawezesha vijana kuonyesha vipaji vyao, hivyo ni vyema sasa Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakawatumia vijana walionesha uwezo kuunda timu ya Mwanza City FC kama ilivyofanya Jiji la Mbeya.
“Ni bora mkaunda timu ya Mwanza City FC ili kushiriki ligi na huenda ikatinga ligi kuu Bara kama walivyofanya wenzetu wa Mbeya na sasa timu ya Mbeya City FC inashiriki ligi kuu, kwani timu zetu kongwe katika Mkoa huu za Toto FC na Pamba FC zimeonekana kuishiwa mbinu za kuwawezesha kurudi ligi kuu,”alisema.
Mganga alisema kwamba mchezo huo mkali ulikuwa ni  wa vuta ni kuvute mashabiki walishuhudia timu hizo zikienda mapumziko  huku zikiwa hazijafungana na katika  kipindi cha pili mchezaji Siraji Juma aliwainua mashabiki kwa kuandika bao la kwanza na bao la pili likifungwa na Paulo Godfrey huku katika hekaheka ya kuokoa mpira ulioelekezwa langoni mwake akijikuta akijifunga na hadi mwisho wa mchezo wadau wa michezo walishuhudia timu ya Mkolani ikitawazwa kuwa mabingwa kwa kuinyuka Mirongo FC bao 2 - 1.
Mashindano hayo ya kombe la Meya 2014 yaliyodhaminiwa na Kampuni ya kutengeneza vinywaji baridi vya Pepsi (SBC), Ndikilo  ndiye aliekabidhi zawadi ya kombe, fedha taslimu  kiasi cha Sh. Ml.1.5,  medali ya dhahabu na Bajaj ya mizigo yenye thamani ya Sh milioni 4.5, mshindi wa pili alinyakuwa Sh milioni 2, kombe dogo na medali ya fedha.
 
Timu ya Sokoni FC iliyoibuka mshindi wa tatu ilijinyakulia fedha taslimu Sh.Mil 1, medali ya shaba na kombe dogo, aidha  mfungaji bora Paulo Godfrey akiwa na bao nane alijinyakulia kiatu cha dhahabu na  fedha kiasi cha sh.200,000.
Aidha   zawadi ya mwamuzi bora  ilikwenda kwa David Albert kutoka Kituo cha Alliance na kupata sh . 200,000  huku timu ya Kata ya Mahina FC ikipata ikiibuka kuwa timu bora na yenye nidhamu na kuondoka na zawadi y ash. 200,000.

No comments:

 
 
Blogger Templates