Social Icons

Monday, April 7, 2014

TIMU YA WATOTO WA MITAANI YA TANZANIA YANYAKUA UBINGWA WA DUNIA NCHINI BRAZIL


  mtaani



Timu ya Taifa ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania jana April 06 imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Dunia wa Watoto wa Mitaani baada kuifunga Burundi mabao 3-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa jijini Rio de Janeiro Brazil.

Mshambuliaji Frank William alifunga mabao matatu katika mechi hiyo iliyochezwa uwanja mkongwe na maarufu wa klabu ya Fluminense huku mgeni rasmi kwenye mechi hiyo akiwa Waziri wa Fedha wa Uingereza George Osborne.

Tanzania ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuitandika Marekani mabao 6-1 ambapo hadi mapumziko ilikuwa mbele kwa mabao 4-0,Burundi ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuifunga Pakistan mabao 4-3 katika mechi ya nusu fainali ya pili.

Timu ya Tanzania inarejea nchini Alhamisi (Aprili 10 mwaka huu) ambapo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 10 jioni kwa ndege ya Emirates.

No comments:

 
 
Blogger Templates