Social Icons

Sunday, April 6, 2014

KUSAIDIA HUDUMA YA DHARURA KWA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO WACHANGA MKOANI RUKWA



Afisa Tawala wa Mradi wa Wazazi na Mwana (MnW) Bwana Mashauri Ndebile akimuonyesha Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Kimanta shehena ya vifaa vya msingi kwa ajili ya kutoa huduma za dharura kwa kina mama wajawazito na watoto wachanga Mkoani Rukwa. Vifaa hivyo mbalimbali vyenye thamani ya Tsh. Milioni 912 vimetolewa kwa Mikoa miwili ya Rukwa na Mwanza, ambapo kwa Mkoa wa Rukwa Mhe.

 Kimanta amevipokea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa huo Injinia Stella Manyanya. Jumla ya Zahanati 172 zitapatiwa vifaa hivyo ambapo kwa Mkoa wa Rukwa ni zahanati 114 kwa Halmashauri za Nkasi na Sumabwawanga Vijijini na Mwanza ni zahanati 64. Vifaa hivyo vimetolewa kwa ushirikiano wa mashirika ya Plan International, Jhpiego na Africare.
Dokta Neema Mamboleo mshauri wa Mradi wa Wazazi na Mwana akimuonyesha Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta kitanda maalum kwa ajili ya kusaidia watoto wachanga waliozaliwa kabla ya muda kutimia na kuwa na matatizo ikiwa ni sehemu ya vifaa hivyo vilivyotolewa na mradi huo. Msaada huo ni sehemu ya misaada mbalimbali ya mashirikia hayo Mkoani Rukwa ambapo hivi karibuni walitoa msaada wa "Ambulance" mbili na kujenga vyumba vya upasuaji kwa Halmashauri za Nkasi na Sumbawanga Vijijini.
Dokta Neema Mamboleo mshauri wa Mradi wa Wazazi na Mwana akimuonyesha Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta kitanda maalum kwa ajili ya kusaidia kinamama wajawazito wakati wa kujifungua.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Hassan Kimanta kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Ndugu Kimulika Galikunga orodha ya mgao wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya Halmashauri hiyo. 
Wadau na wafanyakazi wa Africare Mkoani Rukwa wakiwa katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano. Kulia ni Ndugu Gasper Materu Mratibu wa Africare Mkoa wa Rukwa.
Baadhi ya washiriki wa hafla hiyo.
Picha ya pamoja.
(Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)

No comments:

 
 
Blogger Templates