Social Icons

Sunday, April 20, 2014

BONDIA FRANSIC MIYEYUSHO KUTO SHILIKI MAZOEZI KWA MWEZI MZIMA ILI KULINDA AFYA YAKE



BONDIA Fransic Miyeyusho ' Chichi Mawe' baada ya kupokea kichapo cha mbwa mwizi hivi karibuni na  Bondia Sukkasem Kietyongyuth  kutoka Thailand na kupelekwa hospital na kupatiwa huduma ya kwanza

kwa kufanyiwa uchunguzi wa kina sasa itamlazimu akae pembeni bila kufanya mazoezi ya aina yoyote pamoja na kazi ngumu katika kipindi cha mwezi mzima ili aweze kurudi katika hali yake ya kawaida baada ya kichwa chake kupigwa ngumi nyingi kali kwa mfululizo

akizungumzia mpambano wake huo na mthailand huyo chichi mawe amesema mpambano huu umekuwa ukisogezwa mbele kila wakati na nikibadilishiwa mpinzani kila siku mara ya kwanza mpambano huu ulikuwa ufanyike mwanzoni kabisa mwa mwaka huu ikashindikana nikambiwa nakuja kupigana na  Ronald Pontillas   raia wa Ufilipino nayo ikaota mbawa nikambiwa tena napigana na bondia mwingine pia ikawa hivyo hivyo

ndio nika letewa huyu mthailand kwa sasa ata hivyo mpambano ulikuwa ufanyike april 12 ikasogezwa mbele mpaka april 19 ndipo nilipo panda ulingoni hivyo mpambano ulikuwa na mizegwe sana mana kila siku mkataba ulikuwa ukisogezwa mbele kwa kutumia mkataba hule hule

aliongeza kwa kusema anaomba mashabiki wake wamsamehe kwa kilichotokea kwa kupoteza mpambano huo kwani hata promota mwenyewe alikuwa mbabaishaji na nilikuwa nabadilishiwa ata mapromota mara Jay Msangi mara Mussa Kova hivyo nilikuwa sijui promota alisi ni nani wakati mwanzo nilikuwa namjua msangi

naomba watanzania wenzangu waniombee duwa kwani mchezo kuna kupigwa na kushinda nita hakikisha siwakatishi tamaa
mashabiki wangu pindi nitakapokuwa sawa kwa kurudia ali yangu na kuanza mazoezi

hata hivyo nasikitika kusema mpambano wangu uliokuwa ufanyike mei 10 kuzipiga na Mohamed Matumla nitamuomba promota Ally Mwazoa apeleke mbele kwani sito kubali kupoteza mpambano huo kirahisi najua mwazoa ametumia galama nyingi sana kutangaza mpambano wangu na Matumla sina budi kumuomba msamaha kwa yaliyotokea kwa kuwa yeye ni mwanamichezo na anajua madhala ya mchezo wa ngumi atanielewa kwa kulisogeza pambano hilo mbele

No comments:

 
 
Blogger Templates