Social Icons

Friday, August 9, 2013

WAKALA WA MAJENGO (TBA) KATIKA MAONESHO YA NANE NANE NZUGUNI DODOMA



Wakala wa Majengo (TBA), ulianzishwa mwaka 2002 kupitia Sheria ya Wakala Namba 30 ya mwaka 1997. Lengo la kuanzishwa TBA ni kutoa huduma bora na ya gharama nafuu ya makazi kwa watumishi wa umma na ofisi kwa Serikali na Taasisi zake.

Ikiwa ni taasisi muhumu ya Serikali iliyochini ya Wizara ya Ujenzi, TBA imeshiriki maonesho ya Wakulima maarufu Nane Nane ambayo hii leo yanafikia Kilele katika kanda mbalimbali na Kitaifa yanafikia Kilele katika Viwanja vya Nzuguni, mjini Dodoma.

Timu ya TBA iliyo katika banda lao Viwanja vya Nzuguni jana ilitembelewa na Blog hii na kuikuta ikiwa kamili katika utoaji huduma kwa wananchi ya nini ambacho TBA inakifanya kila siku katika utekelezaji wa shughuli zake.

Timu hiyo pichani kutoka kushoto ni Kaimu Afisa Uhusiano, Mariam Lusewa, Meneja Miradi Maalum, Edwin Nnunduma, Afisa Miliki, Pendaeli Mhufu na Mhandizi Mazingira, Mtapuli Juma.
 Afisa Miliki, Pendaeli Mhufu (kushoto) akihudumia wananchi.
 Wageni wakisaini kitabu cha kutembelea banda hilo na kutoa maoni yao juu ya huduma.
 Kutoka Kulia ni Pendaeli Mhufu, Mariam Lusewa na Mtapuli Juma wakiwa na nyuso za furaha wakati wa kuhudumia wananchi waliotembelea banda lao Nzuguni Dodoma.
 Kaimu Afisa Uhusiano, Mariam Lusewa akiwasikiliza mwananchi  aliyetembelea banda lao jana kupata taarifa mbalimbali.
 Meneja Miradi Maalum, Edwin Nnunduma pamoja na Kaimu Afisa Uhusiano, Mariamu Lusewa wakiwasikiliza wananchi na kuwapa maelezo ama majibu ya maswali yao.
Kaimu Afisa Uhusiano, Mariam Lusewa akimsikiliza mwananchi aliyetembelea banda lao jana kupata taarifa mbalimbali.

No comments:

 
 
Blogger Templates