Social Icons

Wednesday, October 5, 2011

WIZARA YA HABARI KUSHEHEKEA MIAKA 50 YA UHURU BUTIAMA

Na Bebi Kapenya – MAELEZO- Dar es salaam


Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa wiki ya Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo katika maonyesho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara kwenye kijiji cha Butiama mkoani Mara .

Dkt. Nchimbi alitoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati akitoa tamko kwa waandishi wa habari juu ya shughuli mbalimbali zitakazofanyika Kijijini hapo wakati maonyesho ya Wizara hiyo.

Alisema kuwa lengo la maonyesho hayo ni kuwafahamisha wananchi kuhusu mafanikio , changamoto tangu Tanzania bara ipate uhuru katika sekta ya habari, vijana , utamaduni na michezo.

Dkt. Nchimbi aliongeza kuwa maonyesho hayo yatashirikisha Idara, Taasisi na Mashirika yote yaliyo chini ya Wazira Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo kwa kuonyesha machapisho ,picha za tangu uhuru hadi leo zikiwa zinaelezea shughuli mbalimbali za kitaifa na kimataifa ambazo Tanzania imeshiriki na historia ya nchi hii kwa ujumla.

Alisema kuwa katika maonyesho hayo Wizara hiyo itashiriki katika michezo mbalimbali kama vile mchezo wa bao, soka , mpira wa pete , mbio na kuendesha baiskeli ikiwa ni

No comments:

 
 
Blogger Templates