Social Icons

Sunday, October 9, 2011

WAZIRI MAGEMBE AZINDUA BIA YA PILSNER ICE LAGER CLUB MAISHA DAR ES SALAAM USIKU HUU

MFALME WA BIA" PILSNER ICE LAGER YAZALIWA UPYA @ NEW MAISHA CLUB
 Meneja wa Bia ya Pilsner Lager Maurice Njowoka akizungumza machache kabla ya tukio rasmi la kuzindua bia hiyo, ambapo amesema bia hii ni mahususi kwa Vijana na kufafanua kuwa ndio maana hata Brand Manager pia ni kijana hata hivyo amewakumbusha vijana kukumbuka kuwajibika na kutokunywa pombe kwa kupindukia.

 : Pichani Juu na Chini ni Mgeni rasmi Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe akib0nyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa bia hiyo.Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Serengeti Breweries Bi. Teddy Mapunda (wa pili Kulia) Mkurugenzi wa Masoko Bw. Ephraim Mafuru na Brand Manager Pilsner Lager Maurice Njowoka.


 HAPA MWALI AMBAYE NI BIA YA PILSNER ICE LAGER KABLA HAJAZINDULIWA USIKU HUU NDANI YA UKUMBI WA MAISHA CLUB OYSTERBAY DAR ES SALAAM.
MAMBO HAYOO JAMANI BIA YA VIJANA MPOO HAPA IKIFUNGUKA AUTOMATIC BAADA YA ALIYEKUWA MGENI RASMI KUBOFYA.
Mkurugenzi wa Mauzo SBL Bw. Segun Macalauy (kushoto), Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Serengeti Breweries Bi. Teddy Mapunda (katikati) na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya hiyo Ephraim Mafuru wakibadilishana wakati wakimsubiri mgeni rasmi kuwasili pamoja na wageni waalikwaCHEERRRZZZZZZZZZZZZ.
Mkurugenzi wa Mahusiano Teddy Mapunda, katikati Waziri wa Wizara ya Chakula Kilimo na Ushirika Prof.Jumanne Magembe na Mkurugenzi Masoko wa SBL Ephraim Mafuru katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi Masoko wa Kampuni ya Bia Serengeti Ephraim Mafuru akizungumza machache kabla ya kuzinduliwa kwa Bia ya Pilsner Ice Lager ambapo yeye amesema bia hiyo ni mahsusi kwa vijana na ndiyo sababu wamekwenda kuizindua katika ukumbi wa Maisha Club.
Ncha kali akiwa ndiye msema chochote usiku huu wa uzinduzi wa bia ya Pilsner Ice Lager.
   Huyu ndiye Meneja wa Bia  ya Pilsner Ice LagerDavis Njowoka. kama unavyoona Bia ya vijana na Meneja Kijana.

Khadija Kalili nje ya ukumbi wa Maisha Club katika uzinduzi huo uliokuwa mfupi na wenye mvutoo.

No comments:

 
 
Blogger Templates