Social Icons

Wednesday, October 5, 2011

NGUMI KURINDIMA ILALA OKTOBA 16 2011

ZAIDI ya mabondia 42 wanatarajia kushiriki katika mashindano ya mchezo wa ngumi yanayotarajiwa kufanyika Oktoba16 mwaka huu Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kocha wa Klabu ya Ashanti ya Ilala, Rajabu Mhamila, 'Super D' alisema kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha Klabu 12 kutoka katika maeneo mbalimbali.
                   Alisema kuwa mashindano hayo yanatarajia kufanyika katika ukumbi wa Panandi Panandi Ilala.
Super D alisema kuwa mashindano hayo yana lengo la kuhendeleza kuhamasisha mchezo wa ngumi nchini ikiwa ni pamoja na muendelezo wa mchezo huo unanaofanywa na Kinyogoli Foundation.
“Tumeandaa mashindano ya ngumi ambayo yatashirikisha vijana mbalimbali na lengo letu ni kuhamasisha mchezo huo ikiwa ni pamoja na kuuendeleza ili uweze kutuletea faida hapo baaye” alisema.
Kocha huyo alisema kuwa vijana watakaoshiriki watakuwa katika uzito mbalimbali kuanzia Unyoya mpaka uzito wa juu
Alisema kuwa pia wanatarajia kushirikisha mabondia wa kike kutoka katika klabu hizo hizo.Aliongeza kwa kusema kuwa wanaitaji wadau mbalimbali wajitokeze kuwasaidia mahitaji mbalimbali ya vijana ikiwemo maji kwa ajili ya mchezo huo kwa siku hiyo wenye nia ya kutaka kusaidia au kushiliki kwa kuchangia chochote wanaweza kuja katika ukumbi wa mazoezi uliopo Amana Ilala au kufika Klabu ya Ashanti Boxing kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwasiliana na Kocha Mkongwe, Habibu Kinyogoli kwa simu 0655928298.

Au unaweza kuwasiliana na aliyetuma habari na picha  Super D Boxing Coach O713,0787-406938 Email.superdboxingcoach@gmail.com wadau mbalimbali mnakalibishwa

No comments:

 
 
Blogger Templates