Social Icons

Sunday, October 9, 2011

MSANII WA FILAMU BONGO SKYNER ALLY, AFUNGA PINGU ZA MAISHA

 MSANII wa Filamu nchini Skynner Ally mwishoni mwa wiki alifunga pingu za maisha baada ya kufunga ndoa na mumewake Sadi Omar , ndoa ilifungwa nyumbani kwao na bibi harusi Magomeni Dar es Salaam, huku ndoa hiyo ikihudhuriwa na mastaa kibao  wa filamu hapa Bongo akiwemo Irene Uwoya, Johari, Mariam Benny Kinyaiya Mayasa na wengineo wengi.
 
 Msanii nyota wa kike kulia Irene Uwoya nayeye hakubaki nyuma kuwa mmoja kati ya mashuhuda katika ndoa hiyo.
 Bwana na bibi harusi wakinong'onezana jambo ni lipi hilo hiyo ni siri yao.
 Ben Kinyaiya Mayasa na wasanii wengine hawakuwa nyuma katika kutoa pongezi kwa maharusi.
 Hapa Bibi harusi na bwanaharusi wakielekea sehemu maalumu ya kukaa mara baada ya kufunga ndoa yao.
Kila la kheir Skynner na Omar katika maisha yenu ya ndoa.Picha zote kwa hisani ya Mussa Mateja @www.mateja20.blogspot.com

1 comment:

Simon Kitururu said...

Nawatakia kila la kheri kwenye ndoa yenu maharusi!

 
 
Blogger Templates