Social Icons

Tuesday, December 7, 2010

MSHINDI WA PILI TUSKER PROJECT FAME ARUDI NYUMBANI APOKELEWA KWA KISHINDO

Mshindi wa pili wa katika shindano la Tusker Project Fame Peter Msechu mqara baada ya kuwasili leo katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu JK Nyerere, Dar es Salaam.
Akiwa katika gari ambapo aliwapungia mashabiki kuanzia Uwanja wa Ndege,Buguruni, Ilala hadi Mikocheni ambako alikwenda mojakwa moja katika Studio za Redio Clouds kwa mahojiano.

Mkurugenzi wa Mawasiliano , Habari na Uhusiano Mwema wa Ksampuni ya Bia Serengeti (SBL), Teddy Mapunda akibadilishana mawazo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Gonche Materego kabla Msechu kuwasili nchini.
Khadija Kushoto, Mkurugenzi Teddy na Materego katika maongezi ya hapa na pale.
Hili ndilo pipa alilokuja nalo Peter Msechu. Flowers hawa nao walikuwepo kumpa sapoti mchumba wa Peter mwenye Kijani.
Bloggers nao hawakubaki nyuma, Khadija (Bongoweekend),Muhidin Sufian(www.Sufianimafoto.blogspot.com),John Bukuku(www.Fullshangwe.blogspot.com), Ahmad Michuzi (www.Jiachie.blogspot.com)na Musa Mateja yeye anapatikana katika (www.Mateja20.blogspot.com).
Katika hali isiyo ya kawaida kwa wasanii wengi kuficha undani wao hasa wanaojivinjari nao katika mahaba, lakini Peter Msechu amemtambulisha Mupenzi hadharani.
Mwisho akatoa busu motomoto kwa mchumba wake ambaye amemtambulisha mbele ya wanahabari na wote waliofika kumlaki blog hii ilifanikiwa kulinasa jina la binti huyu anaitwa Ammaris K. Muffa.

No comments:

 
 
Blogger Templates