Social Icons

Wednesday, September 29, 2010

VODACOM Miss Tanzania Genevieve Emmanuel aagwa

Vodacom Miss Tanzania 2010, Genevieve Emmanuel Mpangala baada ya kukabidhiwa bendera ya nchi.
Mama mzazi wa Miss Tanzania Genevieve wakiwa na aliyekuwa mgeni rasmi Mwenyekiti wa Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyabiashara Sekta Binafsi nchini Ester Mkwizu na baba yake Emmanuel Mpangala.
Kutoka kushoto ni mlezi wa Miss Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo Cha Uwekezaji nchini (TIC),Emmanuel Ole Naiko,Ester Mkwizu, Genevieve na Mkurugenzi wa Udhamini Vodacom Tanzania George Rwehumbiza.
Akikabidhiwa zawadi ya kinyago, skafu inayolandana na bendera ya nchi pamoja na shanga ya kimasai ya kuvaa shingoni.
Miss Tanzania 2009 Miriam Gerald alikuwepo.
Ester Mkwizu, Genevieve na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Michezo na Utamaduni Profesa Hermans Mwansoko.
Mkurugenzi wa Kituo Cha Uwekezani nchini pia mlezi wa Miss Tanzania akizungumza katika hafla hiyo.
Ofisa Habari wa Kamati ya Miss Tanzania Hidan Rico.
Mkuu wa Itifaki Miss Tanzania Albert Makoye.
Wazazi wa Miss Tanzania wakifuatilia sherehe fupi ya kumuaga mrembo huyo kulia ni Katibu wa Miss Tanzania akifuatiwa na Mdau Yasson Mashaka.
VODACOM Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel Mpangala anaondoka leo kwenda Beijing , China ambako ataingia kambini pamoja na warembo wengine zaidi ya 100 ambao watashiriki katika shindano la kumsaka mrembo wa dunia ‘Miss World’.Akizungumza mara katika hafla fupi ya kuagwa Miss Tanzania Genevieve alisema kuwa ameandaliwa vyema hasa kisaikolojia na Kamati ya Miss Tanzania hivyo hatotishika na kuahidi kuitangaza vyema nchi katika shindano hilo lililopangwa kufanyika Oktoba 30 nchini China.“Nachukua fursa hii kuwaambia Watanzania wote na mashabiki wa fani ya urembo kwa ujumla kuwa nitatumia vyema nafasi yangu ya kuiwakilisha nchi ikiwa ni pamoja na kutangaza utalii, utulivu na amani uliopo nchini na siasa safi kwa ujumla” alisema Genevieve.Aidha mrembo huyo alikabidhiwa bendera na aliyekuwa mgeni rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyabiashara Sekta Binafsi nchini Ester Mkwizu ambaye alimuasa mrembo huyo kuwa yeye ni kioo cha jamii hivyo anapaswa kuwa na nidhamu ya hali ya juu wakati wote.Naye mlezi wa Miss Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo Cha Uwekezaji nchini (TIC) Emmanuel Ole Naiko alimpa zawadi ya makabrasha , kinyago cha mpingo, skafu ya shingoni yenye rangi kama bendera ya nchi pamoja na shanga.Wengine waliokuwepo katika hafla hiyo ni Naibu Katibu Mkuu Profesa Hermans Mwansoko, Mkurugenzi wa Masoko ambao pia ni wadhamini wakuu Vodacom George Rwehumbiza na watu wa kada mbalimbali.Genevieve anakuwa mrembo wa 17 kuwakilisha nchi huku waliomtangulia ni majina na miaka kwenye mabano Aina Maeda(1994), Emily Adolph (1995), Shose Senare (1996), Saida Kessy (1997), Basila Mwanukuzi (1998),Hoyce Temu (1999), Jacqueline Ntuyabaliwe (2000), Happiness Magesse (2001), Angela Damas (2002), Sylvia Bahame (2003),Faraja Kotta(2004),Nancy Sumari (2005), Wema Sepetu (2006), Richa Adhia (2007),Nasrin Karim (2008) na Miriam Gerald (2009).Wakati huohuo Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency ambaye pia ni Mratibu wa Miss Tanzania Hashim Lundenga amesema kwamba mrembo Sala za watanzania zinahitajika kwani anawanawakilisha taifa.
Miss Kinondoni 2010 Alice Lushiku alikuwepo.
Wadau kama kawaida Bongoweekend.

1 comment:

Medahacker said...

hope she wont let us down...

 
 
Blogger Templates