Social Icons

Thursday, September 16, 2010

Kumekucha Tusker Project Fame


Pichani ni Mkuu wa Matukio wa Kampuni ya Serengeti Breweries Bahati Singh (Kushoto), Meneja Uhusiano na Habari Teddy Mapunda na Caroline Nandungu Mshauri Masoko wa Kampuni ya East African Breweries.

Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia kinywaji chake cha Tusker Lager, imezindua rasmi mashindano ya Tusker Project Fame 4 ambapo mshindi atajinyakulia sh. milioni 95 pamoja na kurekodi nyimbo katika studio nchini Afrika Kusini.Mashindano hayo ambayo yanashirikisha nchi za Uganda, Kenya, Tanzania na Rwanda na kuiongeza nchi ya Sudan ya Kusini kwa hapa nchini yatagharimu kiasi cha sh. milioni 300 ambapo wasanii watatu tu wataiwakilisha nchi katika Academy itakayokuwa Kenya.Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano, Habari na Mawasiliano wa kamapuni hiyo, Teddy Mapunda alisema wamezindua rasmi mashindano hayo yenye lengo la kuibua vipaji vya wasanii wa muziki nchini na hata kwa nchi za Afrika Mashariki.Alisema usaili wa mashindano hayo utafanyika Jumamosi Septemba 18, kwenye hoteli ya Peacock Jijini ambapo wasanii wenye zaidi ya umri wa miaka 23 ndiyo watakaoruhusiwa kushindana katika mashindano hayo.''Kwa mwaka huu baada ya kuwafanyia usaili,tunatarajia kupata wawakilishi watatu ambao watakwenda nchini Kenya kwenye hilo jumba maalum la Tusker Project Fame ambapo wataungana na washiriki wengine na kujifunza masuala mbalimbali ya muziki,'' alisema Teddy.Alisema Septemba 25, mwaka huu hiyo kambi itaanza rasmi ambapo wasanii wa hapa nchini watakutana na wasanii wengine 12 kutoka katika nchi hizo na kuanza kushindana rasmi.Pia aliwataja majaji watakaokuwa wakijaji washiriki hao ni Paulo Ndunguru, Sauda Kilumanga na Hamisi Bakari na pia alisema mashindano hayo ni mazuri kwani yaliwatoa wasanii kama Nakaaya Sumari, Hemed na Caroline .Aliongeza kwa kusema jambo kubwa anawaomba Watanzania pindi mashindano hayo yatakapoanza rasmi kujitokeza kwa wingi kuwapigia kura wawakilishi wa hapa nchi kwani kwa kufanya hivyo kutazidi kuwaongezea nafasi za kushinda.Naye Meneja Matukio wa kampuni hiyo, Bahati Sigh alisema tayari promosheni ya mashindano hayo imeshaanza katika baa mbalimbali na pia watafanya promosheni ya barabarani kwa kutumia magari makubwa. Wakati huohuo Mapunda aliongeza kwa kutoa wito kwa Watanzania wenye ndugu na jamaa wenye vipaji vya kuimba wasisite kuwapekeka katika usaili vipaji vya kuimba.Usaili huo umeopangwa kuanza saa2 asubuhi hadi 11 jioni.

No comments:

 
 
Blogger Templates